OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Vikosi vya SMZ vyatakiwa kuongeza kasi ujenzi wa Masoko
HabariHabari Mpya

Vikosi vya SMZ vyatakiwa kuongeza kasi ujenzi wa Masoko

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleimn Abdalla ameviagiza Vikosi vya SMZ vilivyokabidhiwa kazi ya ujenzi wa masoko katika Mkoa Mjini Magharibi kuongeza kasi ujenzi wa miradi hiyo iweze kukamilika ndani ya wakati uliyokusudiwa.

Agizo hilo amelitoa wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Mwanakwereke, Jumbi na  Chuini akiwa pamoja  na  Viongozi  na   mbali mbali  Serikali.

Mhe. Hemed ameeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa masoko hayo ndani ya mwezi mmoja tangu alipofanya ziara yake mwezi mmoja uliopita na kuwataka  waongeze juhudi ili pale atakapotembelea tena mwezi ujao kuwe na mabadiliko makubwa ya ujenzi huo.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais amewapongeza wajenzi  Kikosi cha Chuo cha Mafunzo, Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na Kikosi cha Zima moto na Uokozi kwa  hatua nzuri waliyofikia kwenye miradi hiyo.

Amesisitiza kuwa anamatarajio miradi hiyo itakamilika mapema ili kuiwezesha Serikali kuendelea kutekeleza  miradi mengine mikubwa ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa KItwana Mustafa amesema ujenzi wa masoko hayo unakwenda kutoa nafasi za ajira zaidi ya elfu nne kwa wananchi wa Mkoa wake.

Naye Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar  Khamis Mbeto amemweleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa kama wasimamizi wa Ilani ya CCM wanaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Nane chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.