OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Ofisi ya Mtakwimu yapongezwa kwa kutoa elimu ya matumizi ya Sensa
HabariHabari Mpya

Ofisi ya Mtakwimu yapongezwa kwa kutoa elimu ya matumizi ya Sensa

Mkuu wa Mkoa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa ameipongeza Ofisi ya Mtakwimu Zanzibar kwa kutoa elimu kwa Masheha na Madiwani wa Mkoa huo kuhusu matumizi ya takwimu za sensa ya watu na makaazi ya mwaka  2022.

Pongezi hizo amezitoa alipokuwa akifungua semina juu ya usambazaji wa matokeo na uhamasishaji wa matumizi ya takwimu za sensa hiyo kwa Masheha na Madiwani iliyofanyika ukumbi wa Polisi Ziwani.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo mbali na kuwasidia viongozi hao kupata taarifa  za matokeo ya sensa, vilevile yatawawezesha kupata uelewa kuhusu matumizi ya takwimu za Sensa hiyo. 

Aidha Mkuu wa Mkoa amefahamisha kuwa sensa ndio msingi wa taifa katika kupanga maendeleo yake pamoja na kukuza uchumi wa nchi, hivyo  amewataka Masheha na Madiwani hao kuzitumia takwimu za sensa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Nae Kamishna wa Sensa ya Watu na Makaazi ya mwaka 2022 Balozi Mohammed Hamza  amesema Serikali imetumia fedha nyingi katika kufanikisha sensa hiyo na kuhimiza mashirikiano yaliyooneshwa wakati wa sensa  yaendelezwe katika hatua zote zinazoendelea.

Vilevile Balozi Hamza amesema kuwa taarifa za matokeo ya sensa  zitasaidia Mikoa na Wilaya katika kupanga na kufanya maamuzi ya utekelezaji wa mipango yao mbali mbali ya maendeleo.

Kwa upande wao washiriki wa Semina hiyo wamesema taaluma waliyoipata imeweza kuwajengea uwezo katika matumizi ya sensa,

Takwimu za sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022  zinaonesha Mkoa Mjini Magharibi una idadi ya watu 893,169 sawa na asilima 47 ya watu wote wa Zanzibar ambapo wanawake ni 465,242 na wanaume 427,927.