OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RC arejesha mnada Soko la Makufuli
HabariHabari Mpya

RC arejesha mnada Soko la Makufuli

Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi imeamua kurudisha mnada katika Soko la Wajasiriamali la Makufuli kwa siku za Jumatano na Jumamosi kuanzia wiki ijayo.

Uamuzi huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Soko hilo hapo Makufuli, Wilaya ya Magharibi A.

Amesema uongozi wa Mkoa umefikia uamuzi huo baada ya kutafakari kwa kina maombi ya wafanyabiashara wa Soko hilo ya kuwepo kwa mnada  ili kuvutia wateja na  kupata soko la bidhaa zao kama ilivyokuwa mara tu baada ya kuzinduliwa kwa soko hilo.

Kufuatia uamuzi huo, Mkuu wa Mkoa amesema kuanzia wiki ijayo mnada katika Soko la Jumbi utakuwa ukifanyika siku tano kwa wiki badala ya utaratibu unaotumika sasa.

Aidha ameuagiza uongozi wa Wilaya na Manispaa Magharibi A na Magharibi B kusimamia maamuzi hayo na kuhakikisha kuwa utaratibu huo unaanza  kutumika rasmi wiki ijayo.

Wakati huo huo, Mhe. Idrissa alikabidhi msaada wa shilingi 400,000/= kwa wajasiriamali wawili ili waweze kuendeleza mtaji wao wa bisharara kufuatia ombi lao walilolitoa kwa Mkuu wa Mkoa wakati alipofanya ziara katika soko hilo mapema mwaka huu.

Kwa upande wao Wafanyabiashara  hao wameushukuru uongozi wa Mkoa Mjini Magharibi kwa maamuzi hayo na kusema kuwa wanaimani hali ya biashara itamariaka katika Soko lao.

Soko la Wajasiriamali Makufuli lilijengwa kupitia fedha za UVIKO 19 na kufunguliwa rasmi tarehe 07 Januari, 2023 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Maadhimisho ya Kutimiza Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.