OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Kuapishwa masheha wapya – Mkoa Mjini Magharibi
HabariHabari Mpya

Kuapishwa masheha wapya – Mkoa Mjini Magharibi

Mkuu wa mkoa Mjini Magharibi  Idrissa kitwana  Mustafa amewataka Masheha wa Mkoa huo kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu yao pamoja na kuondoa  changamoto mbali mbali zinazowakabili  wananchi wa Shehia zao

Ameyasema hayo mara baada ya kuwaapisha  masheha  wa Shehia mbali mbali aliyowateua hivi karibuni, hafla iliyofanyika huko  Afisi ya Mkuu  wa  Mkoa  Mjini Magharibi Vuga.

Mkuu wa Mkoa akizungumza baada ya kuapisha masheha wapya

Amesema kuwa bado  kuna kunachangamoto kadhaa katika Shehia zao ikiwemo suala la uhalifu ,wizi , rushwa na vitendo vya udhalilishaji na kuwataka kuchukua hatua za makusudi kupambana na mambo hayo.

Mkuu wa Mkoa  amewataka masheha hao pia kuachana na masuala ya migogoro  ya ardhi  na kutojihushisha katika  migogoro hiyo na kusema kuwa hatasita kuchukua hatua dhidi ya Sheha yoyote atakaebainika kujihusisha na vitendo hivyo. 

Kwa upande mwengine amewataka Masheha hao kutoa huduma kwa wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote na kutofanya upendeleo  katika kutoa huduma muhimu kwa jamii.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa Mjini Magharibi Radhiya Rashid Haroub  amewakumbusha  Masheha kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria, mwongozo na taratibu za kazi zao.

Jumla ya Masheha wa Shehia  saba waliapishwa ikiwemo Mlandege, Shaurimoyo, Mwembeladu, Mwakaje, Welezo, Kianga na Kombeni na kukamilisha safu wa Masheha wa Shehia zote 121 za Mkoa huo.