OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Uteuzi wa Masheha 6 wapya – Mkoa wa Mjini Magharibi
HabariHabari MpyaTaarifa za vyombo vya Habari

Uteuzi wa Masheha 6 wapya – Mkoa wa Mjini Magharibi

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Idrissa Kitwana Mustafa, kwa mujibu wa uwezo aliopewa na Sheria namba 8 ya mwaka 2014 ya Tawala za Mikoa kifungu cha 8 (1), amefanya uteuzi wa Masheha sita wapya katika baadhi ya Shehia za Mkoa huo.

Masheha aliyowateua ni

  1. Ndugu Hamad Barua Kombo – Shehia ya Kombeni
  2. Ndugu Kasongo Omar Kasongo – Shehia ya Mwakaje
  3. Ndugu Muhammad amour Khamis – Shehia ya Welezo.
  4. Ndugu Rajab Asad Mvita – Shehia ya Kianga
  5. Ndugu Hafsa Said Ali – Shehia ya Mlandege
  6. Ndugu Kombo Rajab Kombo – Shehia ya Shaurimoyo

Uteuzi huu umeanza leo tarehe 12 Oktoba, 2021.

Masheha hawa wataapishwa rasmi kushika nyadhifa hizo siku ya Ijumaa tarehe 15 Oktoba 2021 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi ,Vuga