Tovuti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa · Zanzibar
Wasiliana nasi|Dira na DhamiraKiswahili
Nembo ya Serikali ya Mapinduzi ya ZanzibarSERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAROfisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini MagharibiHuduma bora. Uratibu imara. Maendeleo endelevu.
MJINI MAGHARIBIVuga, Zanzibar

Wilaya ya Mjini

Imechapishwa 06.07.2020

Maudhui haya yamehamishwa kutoka kumbukumbu ya tovuti ya 2020–2021. Taarifa za viongozi, takwimu na mawasiliano zinahitaji uhakiki wa sasa.

Wilaya ya Mjini ni  moja kati ya Wilaya mbili (3) za Mkoa wa Mjini Magharibi. Wilaya imepakana na :-

  • Upande wa Kaskazini unapakana na Wilaya ya Magharibi A
  • Upande wa Mashariki Wilaya ya Magharibi B
  • Upande wa Kusini umepakana na Bahari ya Hindi
  • Upande wa Magharibi umepakana na Bahari ya Hindi

Ki Utawala
Wilaya ya Mjini imeundwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Baraza la Manispaa. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya  inaongozwa na Mkuu wa Wilaya akisaidiana na Katibu Tawala .
Baraza la Manispaa linaongozwa na Mkurugenzi akisaidiana na Wakurugenzi wasaidizi kulingana na idara zilizopo ndani ya Baraza la Manispaa.
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inajumla ya idara sita (6) :-

  • Idara ya Mipango Utumishi na Rasilimali watu
  • Idara ya elimu ya maandalizi na msingi
  • Idara ya afya ya msingi
  • Idara ya ustawi wa jamii uchumi na miundombinu
  • Idara ya kilimo, maliasili na mazingira
  • Idara ya Mtambuka

Aidha Wilaya ya Mjini ina majimbo sita 7, ambayo yanafanya wadi 14 na Shehia 34.

Uliza kuhusu taarifa hii
TUKO HAPA KUKUHUDUMIA

Tuijenge Mjini Magharibi pamoja.

Wasiliana nasi ↗