Tovuti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa · Zanzibar
Wasiliana nasi|Dira na DhamiraKiswahili
Nembo ya Serikali ya Mapinduzi ya ZanzibarSERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAROfisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini MagharibiHuduma bora. Uratibu imara. Maendeleo endelevu.
MJINI MAGHARIBIVuga, Zanzibar

Wilaya ya Magharibi "A"

Imechapishwa 06.07.2020

Maudhui haya yamehamishwa kutoka kumbukumbu ya tovuti ya 2020–2021. Taarifa za viongozi, takwimu na mawasiliano zinahitaji uhakiki wa sasa.

Wilaya ya Magharibi “A” ni moja kati ya Wilaya tatu zinazounda Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja iliyo chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali Mitaa na Idara maalum za SMZ. Wilaya ya Magharibi “A” ina majimbo 6, Wadi 10, Shehia 31, Kilomita za mraba 100 pamoja na Baraza moja la Manispaa. Wilaya hii inatekeleza majukumu yake kupitia kamati mbali mbali za Wilaya na Shehia. Katika ngazi ya Wilaya kamati zinazotekeleza majuku ya kiwilaya ni Kamati ya Usalama, Kamati ya Ukimwi, Kamati ya Mazingira, Kamati ya Maafa.
Miongoni mwa majukumu makubwa ya Wilaya ni:

  • Kufuatilia, kusimamia na kuratibu utekelezaji wa shughuli mbali mbali za Serikali ndani ya Wilaya
  • Kuhakikisha kuwa sera, Mipango na miongozo ya Serikali inatekelezwa
  • Kuhakikisha kuwa Sheria na kanuni zinafuatwa katika Wilaya kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.
  • Kuhakikisha kuwa rasilimali zote zinatumika kwa ajili ya kuimarisha uchumi na ustawi wa jamii.
Uliza kuhusu taarifa hii
TUKO HAPA KUKUHUDUMIA

Tuijenge Mjini Magharibi pamoja.

Wasiliana nasi ↗