Tovuti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa · Zanzibar
Wasiliana nasi|Dira na DhamiraKiswahili
Nembo ya Serikali ya Mapinduzi ya ZanzibarSERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAROfisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini MagharibiHuduma bora. Uratibu imara. Maendeleo endelevu.
MJINI MAGHARIBIVuga, Zanzibar

Wilaya ya Magharibi "B"

Imechapishwa 06.07.2020

Maudhui haya yamehamishwa kutoka kumbukumbu ya tovuti ya 2020–2021. Taarifa za viongozi, takwimu na mawasiliano zinahitaji uhakiki wa sasa.

Wilaya ya Magharibi “B”: ni  moja kati ya Wilaya mbili (2) zilizoanzishwa mwaka 2015 kutoka Wilaya ya Magharibi, ambayo ipo ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi. Wilaya imepakana na :-

  • Upande wa Kaskazini unapakana na Wilaya ya Magharibi A
  • Upande wa Mashariki Mkoa wa Kusini / Wilaya ya Kati
  • Upande wa Kusini umepakana na Bahari ya Hindi
  • Upande wa Magharibi umepakana na Wilaya ya Mjini

Ki Utawala
Wilaya ya Magharibi “B” imeundwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Baraza la Manispaa. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya  inaongozwa na Mkuu wa Wilaya akisaidiana na Katibu Tawala .
Baraza la Manispaa linaongozwa na Mkurugenzi akisaidiana na Wakurugenzi wasaidizi kulingana na idara zilizopo ndani ya Baraza la Manispaa.
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inajumla ya idara sita (6) :-

  1. Idara ya Mipango Utumishi na Rasilimali watu
  2. Idara ya elimu ya maandalizi na msingi
  3. Idara ya afya ya msingi
  4. Idara ya ustawi wa jamii uchumi na miundombinu
  5. Idara ya kilimo, maliasili na mazingira
  6. Idara ya Mtambuka

Aidha Wilaya ya Magharibi “B” ina majimbo sita 7, ambayo yanafanya wadi 14 na Shehia 34.

Pia Wilaya ya Magharibi “B” ina jumla ya visiwa vidogo vidogo sita (6) ambavyo hutumika kwa shughuli za uvuvi na utalii. Visiwa vyenyewe ni :-

  1. Kisiwa cha Chumbe kilichopo Chukwani
  2. Kisiwa cha Nguruwe kilichopo Fumba
  3. Kisiwa cha Kwale kilichopo Kumba
  4. Kisiwa cha Sume kilichopo Bweleo
  5. Kisiwa cha Miwi kilichopo Bweleo
  6. Kisiwa cha Ukanga kilichopo baina ya Dimani na Kombeni
Uliza kuhusu taarifa hii
TUKO HAPA KUKUHUDUMIA

Tuijenge Mjini Magharibi pamoja.

Wasiliana nasi ↗