Maudhui haya yamehamishwa kutoka kumbukumbu ya tovuti ya 2020–2021. Taarifa za viongozi, takwimu na mawasiliano zinahitaji uhakiki wa sasa.
Seksheni hii lengo lake ni kutoa huduma za kitaalamu katika nyanja za Mipango, Bajeti na vilevile kuratibu shughuli za Sekretarieti ya Mkoa katika kutoa uwezeshaji wa utaalamu kwa mamlaka za Serikali za Mitaa. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi anayewajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Seksheni ya Mipango na Uratibu:
- Kuratibu suala zima la maendeleo ya kiuchumi kwenye Mkoa ikijumuisha Sekta Binafsi, Mashirika ya Serikali, Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na Asasi za kijamii.
- Kushauri na kuratibu utekelezaji wa sera za sekta mbalimbali katika Mkoa
- Kuratibu maandalizi, usimamizi na tathimini ya mipango (Mpango Mkakati, Mpango Kazi na Bajeti) kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa
- Kuratibu mikutano ya Kamati ya Ushauri ya Mkoa
- Kuchambua, kuunganisha na Kusimamia maandalizi na utekelezaji wa Mpango wa Sekretarieti ya Mkoa na Bajeti
- Kuratibu miradi inayofadhiliwa na wafadhili/wadau wa maendeleo na kushauri shughuli za utekelezaji wa Miradi.
- Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa kuhusu shughuli na majukumu ya mashirika, taasisi za kijamii na sekta binafsi
- Kushauri na kuratibu shughuli za utafiti katika Mkoa
- Kuratibu mazoezi ya sensa ya watu na makazi
- Kuratibu shughuli zitokanazo na majanga katika Mkoa
- Kuzisaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuandaa maandiko ya miradi
- Kuratibu utekelezaji au ushughulikiaji wa masuala mtambuka ikijumuisha masuala ya Jinsia, Ulemavu, HIV/AIDS, na Kuwa mratibu au msimamizi wa masuala ya Jinsia katika Mkoa.
- Kuratibu utekelezaji na kusimamia ushiriki wa sekta binafsi katika masuala mbalimbali ya maendeleo
- Kusimamia na kutathimini utendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa.
