Maudhui haya yamehamishwa kutoka kumbukumbu ya tovuti ya 2020–2021. Taarifa za viongozi, takwimu na mawasiliano zinahitaji uhakiki wa sasa.
Seksheni hii ina lengo la kutoa huduma za kitaalamu zinazohitajika kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza Miundombinu na inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Seksheni ya Miundombinu:
- Kuratibu utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Viwango katika nyanja za Barabara, Majengo, Upimaji, Ardhi na Mipangomiji
- Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika nyanja za Barabara, Majengo, Upimaji, Ardhi na Mipangomiji
- Kuwasiliana/kuwa daraja kuunganisha baina ya Mamlaka zinazohusika kwenye Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya masuala ya Ujenzi
- Kushauri juu ya Masuala ya barabara, Ujenzi, Viwanja na uboreshaji mifumo
- Kusimamia na kushauri juu ya kazi za Ujenzi zinazotekelezwa ndani ya Mkoa
- Kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kutwaa ardhi kwa ajili ya matumizi ya Serikali Kuu
- Kuandaa ramani kwa ajili ya mipangomiji
- Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa juu ya Tathimini ya Athari za Kimazingira
