Maudhui haya yamehamishwa kutoka kumbukumbu ya tovuti ya 2020–2021. Taarifa za viongozi, takwimu na mawasiliano zinahitaji uhakiki wa sasa.
Seksheni hii lengo lake ni kuwezesha utoaji wa huduma bora za Afya za kinga, matibabu na maendeleo ya huduma za Afya na Ustawi wa Jamii katika Mkoa. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa, ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Seksheni ya Ustawi wa Jamii:
- Kuratibu na kushauri juu ya utekelezaji wa wa sera za Afya katika Mkoa
- Kuratibu masuala ya Afya na Ustawi wa Jamii katika Mkoa
- Kusimamia utoaji sahihi wa huduma za Afya zinazotolewa na hospitali/vituo vya Umma na sekta binafsi katika Mkoa
- Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utoaji wa huduma za Afya
- Kutoa ushauri wa kitaalamu katika uandaaji wa mipango ya upambanaji/uzuiaji wa tatizo la Virusi/UKIMWI (HIV/AIDS)
- Kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uendeshaji wa shughuli zinazohusiana na masuala ya Virusi/UKIMWI (HIV/AIDS) katika Mkoa
- Kutoa huduma za Afya/msaada unaohitajika wakati wa milipuko ya magonjwa katika Mkoa
- Kutoa huduma za kliniki na matibabu kwa wagonjwa wa ndani na nje wanaoletwa kutoka vituo vya Afya/hospitali za mamlaka za Serikali za Mitaa.
- Kutoa huduma za kitaalamu (utaalamu wa kubobea) za matibabu
- Kutoa/Kusaidia huduma za kitaalamu na msaada unaohitajika kwa vituo vya Afya na Hospitali za Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa milipuko ya magonjwa yakuambukiza
- Kutoa huduma za rufaa za maabara na vipimo
- Kuratibu upatikanaji wa madawa/vifaa tiba kwa ajili ya hospitali.
