Mkuu wa wilaya ya Magharibi ‘A’ Abeid Juma Ali, amesisitiza umuhimu wa wazazi kuwalina na kusimamia ulinzi wa watoto wao katika kipindi hiki taifa likiwa katika vita dhidi ya maradhi ya corona.
Akizungumza katika pwani ya Mangroove katika shehia ya chuini wilayani humo, mkuu huyo wa wilaya alieleza kuwa serikali imepiga marufuku mikusanyiko na kuzuia shughuli zote zenye mikusanyiko zikiwemo za elimu ili kuzuia kuenea kwa virusi vya maradhi hayi hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutii maagizo hayo.
Alisema iwapo kila mzazi atatekeleza wajibu wake kikamilifu, kuna uwezekano mkubwa wa kuzuiwa kasi ya maambukizo ya ugonjwa huo ambao hadi sasa Zanzibar imethitisha kuwepo kwa wagonjwa watatu.
“Serikali inapotoa maelekezo mjue kuwa hiyo ni amri na inapaswa kutekelezwa, kusimamiwa na kutiiwa na kila mmoja wetu. Hivyo kuanzia leo (jana) sitaki kuona mtu anakuja kuogelea katika eneo hili hadi hali itakapokuwa shwari kwani katika kipindi hiki ni hatari kwenu,” alieleza DC. Abeid.
