Tovuti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa · Zanzibar
Wasiliana nasi|Dira na DhamiraKiswahili
Nembo ya Serikali ya Mapinduzi ya ZanzibarSERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAROfisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini MagharibiHuduma bora. Uratibu imara. Maendeleo endelevu.
MJINI MAGHARIBIVuga, Zanzibar

Mkakati wa Uvaaji Barakoa

Imechapishwa 27.07.2020 · Habari Mpya

Maudhui haya yamehamishwa kutoka kumbukumbu ya tovuti ya 2020–2021. Taarifa za viongozi, takwimu na mawasiliano zinahitaji uhakiki wa sasa.
Mkakati wa Uvaaji Barakoa

SERIKALI ya Mkoa wa Mjini Magharibi imeandaa mkakati maalum wa kusimamia maelekezo na maagizo ya serikali ya kuvaa barakoa na kutumia vitakasa mikono kwa wananchi mbali mbali wanaoingia katika mkoa huo.

Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama na viongozi wa mkoa huo mwenyekiti wa kamati ya usalama ya mkoa Mjini ambae pia ni mkuu wa Mkoa huo Mhe Hassan Khatib amesema kwa serikali ya mkoa huo haitawavumilia watu na watoa huduma walipo na wanaoingia katika mkoa huo bila ya kuvaa barakoa.

Amesema serikali ya mkoa imekuwa ikichukua juhudi mbali mbali za kueleimisha na kuhamisisha juu ya uchukuaji wa tahadhari kwan jamii dhidi ya kujikinga na maambukizi ya maradhi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virus vya corona.

“ Tumekuwa tukichukuwa juhudi mbali mbali za kupita katika maeneo yetu kutoa taaluma lakini kama haitoshi pia matangazo kwenye vyombo vya habari tunatoa,hivyo sasa tuchukua hatua kwa kila atakaeingia katika mkoa huu bila ya barakoa.

Aidha mkuu wa mkoa amesema pamoja na mambo mengine atahakikisha anashirikiana na viongozi wa wilaya na manispaa za mkoa huo kuangalia uwezekanao wa kugawa barakoa kwa wananchi wa mkoa huo huku ikizingatia makundi maaalum.

Hata hivyo Mhe Hassan amesisitiza serikali ya mkoa wake inadhamiria kulinda mipaka yake kwa kupima joto wananchi wanaoingia na kutoka katika mkoa huo ili kuona jamii inaendelea kuwa salama na maambukizi ya maradhi ya covid-19.

Nao wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wamesema pamoja na kazi nzuri inayofanywa na viongozi wa mkoa na wilaya katika mapambano ya maradhi ya corona lakini kunahitajika nguvu ya ziada katika kuwasimamia wananchi kuhusu  uvaaji wa barakoa.

“Mhe Mwenyekiti tunaoziona juhudi mbali mbali zinachukuliwa hasa katika suala la utoaji elimu lakini pia usimamizi wa maagizo ya serikali mkupitia wataaalamu wa afya,kikubwa ni kuongeza juhudi katika kuwasimamia wananchi kuvaa barakoa hususani wale waliokuwa wakaidi”walisema wajumbe hao.

Kikiao hicho cha kamati ya ulinzi na usalama kimeazimia kugawa barakoa kwa wananchi mbali mbali wa mkoa huo kwa kuwatumia masheha na madiwani,kupima joto wananchi wanaoingia na kutoka katika mkoa huo pamoja na kuhakikisha kila mwananchi na wanotoa huduma katika mkoa huo anavaa barakoa.

Uliza kuhusu taarifa hii
TUKO HAPA KUKUHUDUMIA

Tuijenge Mjini Magharibi pamoja.

Wasiliana nasi ↗