Kazi ya ujenzi wa barabara mpya za mjini ikiwa imeanza katika barabara ya Nyerere eneo la Mnazi mmoja.
Zaidi ya kilomita mia moja ya barabara pamoja na barabara za juu (flyover), zitajengwa katika mradi huo mkubwa unaokwenda kubadilisha mandhari ya mji.
Mradi huo unatekelezwa na Kampuni ya CCECC kutoka China.
Kuanza kwa ujenzi wa mradi huu kunafuatia ahadi aliyoitoa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kuzijenga barabara zote kuu za Mjini, Mkoa Mjini Magharibi.