Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amewataka Wakaazi wa Mji Mkongwe kuchukua tahadhari dhidi ya miripuko ya moto amesema hayo wakati alipotembelea kwenye eneo la tukio la kuungua moto nyumba katika Sheha ya Kiponda Mkoa wa Mjini Magharibi na kutoa pole kwa familia zilizo athirika .
Aidha ametoa pole kwa familia ya marehemu Bi Rehema Chande Chande ambae alifariki alipokuwa akijihami akiwa amembeba mjukuu wake Nabili Issa Ramadhani mwenye umri wa miaka 5, ambae yupo hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kwa matibabu zaidi.
Nae shuhuda wa tukio hilo Bw. Seif Omar Hamad amesema Chanzo cha moto huo ni hitilafu za vifaa vya umeme katika Nyumba ya marehemu na kupelekea kuvunja Nyumba hali iyopelekea kujitupa kutoka juu hadi chini kwa kuokaa maisha ya mjukuu wake na kupelekea kifo chake aidha amesema chanzo hicho kutokana na kukosekana kwa msaada wa haraka.
Nae Sheha wa Shehia hiyo ambae pia Muathirika wa tukio hilo Mh.Juna Khamis Makame amesema marehemu Bi Rehema Chande Chande amepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 71. Marehemu alikuwa anakaa Nyumba nambari 1508 Kiponda zaidi ya vyumba 7 vimeathirika na moto na hakuna thamani wala kifaa chochote kilichopatikakana, Pia nyumba ya jirani nambari 1509 yenye familia 3 imeathirika.
Katika eneo hilo la tukio limehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya, Mstahiki Meya, Katibu Tawala Mkoa na Wilaya ya Mjini, Kamishina wa Zimamoto, Maafisa wa Polisi, Madiwani, Masheha na Wananchi.