OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Mkuu wa Mkoa awashukuru Mashekh
HabariHabari Mpya

Mkuu wa Mkoa awashukuru Mashekh

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amewashukuru mashekh kwa namna walivyoutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani  kwa kutoa elimu ya dini pamoja na kugusia mambo ya kijamii katika darsa na   matukio mbali mbali yaliyofanyika ndani ya mwezi huo.

Ametoa shukurani hizo wakati akizungumza na Mashekh na Maimamu wa misikiti mbali mbali hapo afisini kwake Vuga.

Ameeleza kuwa Serikali ya Mkoa  imefarajika na namna viongozi hao mbali ya kutoa elimu ya dini vilevile wameweza  kuiasa jamii kuachana na mambo ya udhalilishaji na yanayoenda kinyume na silka na utamaduni wa  wazanzibari.

Aidha amewaomba viongozi hao kuendelea kuikumbusha jamii juu ya umuhimu wa kutenda mambo mema, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa ameishukuru pia Ofisi ya Mufti kwa kusimamia vyema shughuli mbali mbali za kidini yakiwemo mashindano ya kuhifadhi Qur-an, kutoa sadaka na darsa yaliyofanyika ndani ya Mkoa huo katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Naye Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar Shekh Khalid Ali Mfaume amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa Ofisi yake itaendelea kusimamia shughuli za kidini nchini ili kuhakikisha jamii inaendelea kuwa kitu kimoja.