OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Mianya ya Udhalilishaji wa Kijinsia Yabainika.
HabariHabari Mpya

Mianya ya Udhalilishaji wa Kijinsia Yabainika.

Uongozi wa  Mkoa Mjini Magharibi umeahidi kutoa kila aina ya mashirikiano kwa Kamati ya Kuzuia Udhalilishaji wa Kijinsia  ili kuhakikisha dhamira ya Serikali kuunda Kamati hiyo inafikiwa.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo Idrissa Kitwana Mustafa amesema hayo alipokutana na Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mwanamkaa Abdulrahman Mohammed walipofika Ofisini kwake Vuga.

Ameieleza kamati hiyo kuwa Mkoa upo tayari kuchukua hatua dhidi ya mianya waliyoibaini kuwa ikisababisha kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwenye Mkoa huo.

Aidha Mkuu wa Mkoa ameipongeza Kamati hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya na kusema kuwa wameisaidia Serikali kuweza kuongeza juhudi katika kupambana na vitendo hivyo. 

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kuzuia Udhalilishaji wa Kijinsia Mwanamkaa Abdulrahmn amesema Kamati yake imegundua mianya mbali mbali katika jamii ambayo inapelekea vitendo vya udhalilisha kuongezeka.

Amesema kwamba wameamua kukutana na viongozi wa Mikoa, Wizara na Taasisi mbali mbali kwa ajili ya kuwaleza juu ya mianya waliyoigundua ili kuangalia namna watakavyoweza kuzuia mianya hiyo.

Kamati hiyo ilizinduliwa  tarehe 1 Juni, mwaka huu na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa lengo ni kuzuia mianya inayopelekea matukio ya udhalilishaji inajumuisha wajumbe kutoka Wizara na taasisi mbali mbali za Serikali, zisizo za kiserikali, viongozi wa dini na NGOs.