OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Masheha Watakiwa Kufanya Kazi kwa Mashirikiano
HabariHabari Mpya

Masheha Watakiwa Kufanya Kazi kwa Mashirikiano

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amewataka Masheha wa Mkoa huo kuongeza mashirikiano katika utendaji wa kazi zao.

Amesema mashirikiano baina yao ndio njia pekee itakayoweza kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi pamoja na kufanikisha masuala mbali mbali ya Serikali yanayotekelezwa ndani ya Shehia zao.

Mkuu wa Mkoa amesema hayo mara baada ya kuwaapisha masheha wapya aliyowateua hivi karibuni katika Shehia kadhaa za Mkoa huo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” Suzan Kunambi amesema kazi ya Masheha ni kuwahudumia wananchi hivyo amewataka kutimiza wajibu wao kikamilifu.

Amesema yapo mambo ambayo Masheha wangeweza kuyafanyia kazi na kuyapatia ufumbuzi badala ya kuwaelekeza Wananchi kuyapeleka ngazi ya Wilaya na Mkoa.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Moh’d Ali Abdalla amewahimiza Masheha kufanya kazi kwa kufuata Sheria katika kutekeleza wajibu wao.

Masheha waliyoapishwa ni Mohammed Mussa  Machano Shehia ya Kwahani, Omar Juma Masoud Shehia ya Kihinani na Khamis Bakari Juma Shehia ya Kama.