OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>NGOs zatakiwa zisimamie malengo yao
HabariHabari Mpya

NGOs zatakiwa zisimamie malengo yao

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amekutana na kufanya mazungumzo na Jumuia ya Kupiga vita Rushwa na Uhujumu Uchumi  Zanzibar (JUKURUZA), walipofika ofisini kwake Vuga kujitambusha.

Mkuu wa Mkoa amewapongeza viongozi wa Jumuia hiyo kwa kuamua kuunda chombo hicho chenye azma ya kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mapambano dhidi ya rushwa na uhujumu uchumi.

Ameitaka Jumuia hiyo  kuhakikisha kuwa wanasimamia dhamira ya kuundwa kwa chombo hicho ili malengo waliyojiwekea waweze kuyafikia .  

Mhe. Idrissa amewatanabahisha  kuwa kumekuwepo na mtindo kwa baadhi ya watu kuanzisha Jumuia kwa nia njema ya kuisaidia jamii lakini hatimaye huacha malengo ya kuanzishwa kwa Jumuia hizo na kujiingiza katika mambo ambayo yanakiuka sheria na taratibu za nchi.

Mwenyekiti wa JUKURUZA  Khalfan Ali Faki amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa  dhamira ya kuanzishwa kwa  Jumuia hiyo ni  kupiga vita vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi katika ngazi mbali mbali na ameomba kupatiwa mashirikiano ya Mkoa, Wilaya na Shehia katika kutekeleza shughuli zao.