Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Mohd Ali Abdalla amewataka Wakandarasi wa miradi ya fedha za Uviko19 kufanya juhudi ya kumaliza miradi hiyo kama serekali ilivyoagiza
Amesema licha ya hatua kubwa walizofikia bado wanatakiwa kuongeza bidii ili kukamilisha hatua iliyobakiza.
Katibu Tawala ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa majengo ya wajasiriamali katika Wilaya ya Mjini , Magharibi A na Magharibi B
Akiwa ameambatana na Mafisa mbali mbali waandamizi wa Mkoa huo, Mohd amesema miradi hiyo itakapokamilika itawawezesha wajasiriamali kufanya kazi zao katika maeneo bora zaidi.
Ameongeza pia ujenzi huo utaondoa changamoto inayowakabili wajasiriamali kwa kufanya biashara katika maeneo yasio rasimi.
Nae Muhandisi Msimamizi ndugu Salum Masoud amesema ujenzi wa majengo hayo umefikia asilimia tisini na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni
Miradi aliokagua ni Majengo ya wajasiriamali Mombasa ,Welezo na Masumbani