OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Viongozi Manispaa fanyeni kazi kwa mashirikiano – RAS Mjini Magharibi
HabariHabari Mpya

Viongozi Manispaa fanyeni kazi kwa mashirikiano – RAS Mjini Magharibi

Imeelezwa kuwa mashirikiano ya karibu baina ya Manispaa na  Jiji ndio njia pekee itakayopelekea kuleta ufanisi wa kazi. .

Katibu Tawala Mkoa wa Mjini Magharibi Mohamed Ali Abdallah amewataka Mamea na Wenyeviti wa Kamati za Mabaraza ya Manispaaa kufanya kazi kwa mashirikiano ya karibu ili kuleta ufanisi wa kazi na kufikia malengo ya taifa.

Bwana Mohamed ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakati alipokutana na viongozi hao katika Kikao kazi cha kujadili mwenendo wa uwajibikaji wa Manispaa hizo ndani ya Mkoa huo.

Amesema kumekuepo kwa mwenendo usioridhisha wa kufanya kazi bila ya mashirikiano kwa Manispaaa hizo jambo ambalo halileti taaswira nzuri na kupelekea kushindwa kufikia malengo ya Serikali katika kuwahudumia wananchi wake.

Aidha ameongeza kuwa  kusipokuepo kwa mahusiano ya kutosha ya ndani Mabaraza hayo yatashindwa kufanya kazi zake nyema na kushindwa kumsaidia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika  mipango yake ya maendeleo na malengo aliyoyakusudia hapa nchini.

Akizungumzia kuhusu hali ya mvua zinazoendelea kunyesha amewaagiza viongozi wa Mabaraza ya Manispaaa hizo kusimamia vyema suala la usafi ili kujiepusha na majanga ya magonjwa ya miripiko.

Nao Mamea na Wanyeviti wa kamati za Manispaa hizo wameahidi kujipanga upya katika kutekeleza majukumu yao na kuahidi kufanya kazi kwa mashirikiano huku wakieleza  utayari wao katika kuondoa changamoto zote zilizopo akiwemo kutekeleza maagizo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wakuu wa nchi

Kikao kazi cha kwanza kilichoandaliwa na Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi kiliwahusisha  Wakurugenzi, Mamea na Wenyeviti wa kamati za Mabaraza ya  Manispaa hizo  kitafanyika kila baada ya miezi mitatu kwa lengo la kupima hatua za uwajibikaji.