Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mhe Mahmoud Muhammed Mussa amesema Baraza la Jiji la Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi zinazoshughulika na masuala ya Usafi litahakikisha Mji wa Zanzibar unabaki katika hali ya usafi na kufikia Zanzibar “Taka Ziro” ili kuondokana hali hatarishi kwa wananchi wake.
Mstahiki Meya amesemahayo leo alipokua na kikao cha pamoja kati ya Taasisi ya Wanaharakati wa mazingira na shughuli za jamiii (YEACODO) na YONA Zinazofanya kazi zao kwa kushirikiana na Baraza la Jiji la Zanzibar na watendaji wa Watendaji wa Baraza hilo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Baraza la Jiji zilizopo Michenzani Mall.
Aidha Mstahiki Meya amesema katika kutekeleza hilo tayari kumeandaliwa utaratibu maalum wa kuufanya Mji wa Zanzibar ikiwa pamoja wa kuvisogeza karibu vikundi vya usafi ili waweza kufanya kazi kwa pamoja na kujua changamoto zao kwa kuangalia namna gani wanaweza kuweka safi Jiji la Zanzibar.
Hata hiyo Mstahiki Meya amezitakaTaasisi hizoo kuendelea na juhudi za kuinguka mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Azma yake ya kuuweka mji katika hali ya ubora unaotambulikana kimataifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya YEACODA Ibrahim Salum Hussein amesema lengo la kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kuona Zanzibar inabaki kuwa na ubora unaotakiwa na hadi sasa zaidi ya vikundi 40 vya usafi wanashirikiano navyo katika kutimiza maelengo hayo.
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya YONO AUCTION MARK Abdalla Ali Makame ameahidi kutoa mashirikiano katika Afisi za Baraza la Jiji ili kuhakikisha Zanzibar inafikia Zanzibar “Taka Ziro”
Wakichangia Mada baadhi ya wajumbe na watendaji wa Baraza la Jiji wamesema ni vyema kwa taasisi hiyo kujipanga zaid na kutafautisha baina ya taka ngumu na taka nyepesi ili zoezi lao liweze kufanikiwa zaidi.