OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Dkt. Mwinyi. TAMISEMIM  limalizeni kero la upigwaji muziki
HabariHabari Mpya

Dkt. Mwinyi. TAMISEMIM  limalizeni kero la upigwaji muziki

Wizara ya Nchi (OR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mikoa na Manispaa wametakiwa kuhakikisha wanalipatia ufumbuzi wa kudumu kero la upigaji wa muziki kwenye maeneo ya makaazi ya watu na Hoteli za kitalii.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa agizo hilo kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mmoja ya wawekezaji katika Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara la Zanzibar uliofanyika Hoteli ya Golden Tulip, Kiembesamaki.

Amesema kero hiyo imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu na wananchi pamoja na wawekezaji, hivyo amezitaka Taasisi zote husika kuishughulikia na kumpatia taarifa ya utekelezaji wake ndani ya muda mfupi.

Amesema Serikali haipingi biashara hiyo, hata hivyo lazima sheria na kanuni zifuatwe na watu watakaopewa vibali vya kupiga  muziki wapige katika kumbi zisizotoa sauti ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.

Aidha Dkt. Mwinyi ameagiza pia kulishughulikia suala la vitendo vinavyoenda kinyume na maadili katika maeneo yaliyo karibu na kumbi za kupiga muziki na bar.

Katika mkutano huo mmoja wa wawekezaji alilalamikia kero ya upigaji wa muziki kwa sauti kubwa, uwepo wa bar zisizo na vibali na vitendo vinavyoenda kinyume na maadili katika maeneo yaliyo karibu na Hoteli za kitalii.