Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mheshimiwa Idrissa Kitwana Mustafa amesema uwepo wa umeme wa Sola atasaidia kupunguza changamoto zilizopo za umeme wa kawaida.
Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo huko Gulioni katika ghafla ya uzinduzi wa mradi wa Sola Maisha Bora wakati alipokua akitoa salamu za wananchi wa Mkoa wake.
Amesema umeme ni uhai na ni maisha Bora yenye kujenga uchumi na ustawi wa watu ambapo sehemu ambayo haina umeme hakuna maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hivyo ujio wa umeme huo wa Sola atasaidia kupunguza tatizo liliopo la umeme ndani ya Mkoa wa mjini Magharibi na Zanzibar kwa ujumla.
Aisha Mheshimiwa Idrissa amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa juhudi zake za kuwaletea Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar.