OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>RC Mjini Magharibi awataka vijana kufanya utalii wa ndani
HabariHabari Mpya

RC Mjini Magharibi awataka vijana kufanya utalii wa ndani

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh.Idrissa Kitwana Mustafa amesema kunahaja ya vijana kuijuwa historia ya Zanzibar kuliko wageni kutoka nje kwa maendeleo ya vizazi vya sasa na baadae.

Aidha amesema Zanzibar ina maeneo mengi ya vivutio vya Utalii ambavyo vijana wanapaswa kuvifahamu.

Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo Cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na wadau wa utali kwenye ufunguzi wa tamasha la utalii huko Chuo Cha Utali Maruhubi.

Mkuu wa Mkoa amesema tamasha hilo litautangaza  utamaduni wa Mzanzibar na vivutio vyake na kuingiza watalii wengi kutoka nje ya Zanzibar.

Aidha Idrissa  ameitaka Idara ya Utali na  Mambo ya Kale kuunga mkono jitihada za wanafunzi kwenye  kuutangaza utalii nchini.

Amewataka vijana na wasomi kuwa wazalendo na kutumia mitandao ya kijamii kuonesha vivutio vya utalii na kuitambulisha Zanzibar ikiwa ndio adhma ya uchumi wa bluu na filamu ya Royal tour.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Utalii na Mambo ya Kale Dkt Abdullah Mohamed Juma  kwa niaba ya Wizara  hiyo amesema vijana wanahitajika kujuwa  utalii wa ndani kuliko wageni kutoka nje ya Zanzibar.

Rais wa Serekali ya wanafunzi SUZASO Ndg. Said Azan ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kujali juhudi za Serekali ya wanafunzi na kuiomba kuzidisha ulinzi na usalama wa Mkoa Mjini Magharibi Ili kuengeza idadi ya watalii Zanzibar.

Tamasha la utalii kimataifa Zanzibar limeandaliwa na Serekali ya wanafunzi SUZASO na kuhudhuriwa na watendaji wa Serekali, wadau wa utalii, wanafunzi na taasisi binafsi.