Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amewaapisha Masheha wa Shehia tano za Mkoa huo aliwateua tarehe 14/12/2023.
Masheha aliowaapisha kwa Wilaya ya Mjini ni Maryam Laban Elijah Shehia ya Mpendae, Habiba Mussa Mohamed Shehia ya Migombani, na Munir Ali Yussuf Shehia ya Mkunazini.
Kwa Wilaya ya Magharibi ‘A’ waliyoapishwa ni Juma Sheha Khamis Shehia ya Kwa Goa na Haji Maabad Haji Shehia ya Mtopepo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa amewahimiza Masheha kuwa karibu na wananchi katika kuwapatia huduma mbali mbali.
Amesema Serikali imewapa nafasi hiyo ikiamini wanao uwezo wa kuwahudumia wananchi pamoja na kutekeleza shughuli za Serikali.
Mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha pia Masheha hao kuzingatia maadili na kuwa weledi katika kufanya kazi zao mbele ya jamii.