OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Serikali kujenga viwanja vya michezo kila Wilaya na Mkoa
HabariHabari Mpya

Serikali kujenga viwanja vya michezo kila Wilaya na Mkoa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kwamba Serikali itajenga viwanja vya kisasa vya michezo kila Wilaya na Mkoa pamoja kuufanyia ukarabati mkubwa uwanja wa Amani.


Amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la uwanja wa michezo unaojengwa matumbaku.

Dkt. Mwinyi amesema viwanja hivyo vitajumuisha michezo ya aina mbali mbali ili kutoa fursa pana kwa vijana kuweza kushiriki michezo.
Aidha amesema Serikali inapata faraja kuona inatimiza miaka 59 ya Mapinduzi kwa uwekaji wa mawe ya msingi na uzinduzi wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa sekta mbali mbali na kuwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali yao.

Akitoa salamu za wananchi katika shughuli hiyo, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa  amasema Mkoa utaendelea kushirikiana na Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na michezo ili kufanikisha miradi yote iliyokusudiwa kutekelezwa ndani ya Mkoa wake katika sekta ya michezo.

Naye Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya amesema mbali na miradi ya fedha za UVIKO, ipo miradi   kadhaa inayotekelezwa kwa fedha za Serikali ukiwemo ujenzi wa uwanja huo wa michezo uliogharimu shilingi bilioni 1.1

Viongozi mbali waliopata fursa ya kuzungumza  wamempongeza Rais wa Zanzibar kwa utekelezaji wake wa miradi ya maendeleo kama inavyoelekeza ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2025

Uwanja huo utakuwa na  viwanja vinne vya mpira wa miguu pamoja na michezo mengine, jengo la vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo, vyoo na jukwaa la watazamaji unatekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).