Idara hii ina lengo la kuziwezesha Idara nyingine kutimiza majukumu yake, kutoa utaalamu na huduma mbalimbali zinazohusiana na usimamizi wa Rasilimali watu na Utawala kwenye Sekretarieti ya Mkoa. Idara hii inaongozwa na Afisa Mkuu Utawala na Rasiliamali watu ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Idara ya Utawala na Rasilimali Watu:
- Kuratibu masuala ya Mahusiano na Ustawi wa Wafanyakazi ikiwa na pamoja na masuala ya Afya, Usalama kazini, na Utamaduni
- Kuratibu maandalizi, utekelezaji, usimamizi na tathimini ya Mkataba wa Huduma kwa Umma kwenye Sekretarieti ya Mkoa
- Kutoa huduma za Masijala, na usimamizi wa kumbukumbu
- Kutoa huduma za Itifaki katika Mkoa
- Kuratibu huduma za Ulinzi, Usafi na utunzaji Ofisi, majengo na maeneo/viwanja vya Ofisi na huduma za Usafiri
- Kushirikiana na Tume ya Utumishi wa Umma yanayohusiana na Ajira na Uteuzi wa watumishi.
- Kusimamia hatua/Mchakato wa kuwathibitisha na kuwapandisha vyeo/madaraja watumishi wa Mkoa
- Kuwezesha mafunzo ya rasilimaliwatu na maendeleo (taaluma, weledi, kuboresha ujuzi) kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa
- Kuwezesha programu za mafunzo elekezi kwa waajiriwa/watumishi wapya
- Kusimamia Mpango wa Rasilimaliwatu kwa ajili ya kujua upatikanaji na mahitaji ya wataalamu kwenye Sekretarieti ya Mkoa
- Kusimamia mishahara na kushauri juu ya kusimamia mfumo/orodha ya malipo ya mshahara
- Kusimamia utekelezaji wa mfumo wa wazi wa mapitio na upimaji wa utendaji wa kazi (OPRAS)
- Kushughulikia na kuhuisha taarifa za watumishi kama Likizo za mwaka, likizo za uzazi na matibab, ruhusa za mafunzo/masomo na watumishi kuondoka kazini
- Kuratibu upatikanaji wa mafao ya watumishi (malipo ya pensheni n.k) na madai mengineyo
- Kushughulikia upatikanaji wa huduma zinazohusiana na watumishi kuondoka kwenye utumishi (kustaafu, kujiuzulu n.k)
- Kusimamia masuala ya kinidhamu kwa wafanyakazi wa Mkoa
- Kuratibu na kushughulikia malalamiko na mashitaka ya wafanyakazi wa Mkoa
- Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa juu ya masuala yanayohusu rasilimaliwatu
- kuratibu utekelezaji wa sera ya Utumishi wa Umma na sheria kanuni na miongozo inayohusiana naa Utumishi wa Umma.