- Kitengo hiki kina lengo la kutoa huduma ya ushauri kwa Afisa Masuuli kuhusu taratibu sahihi na zinazokubalika za usimamizi wa masuala ya fedha. Kitengo hiki kinaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Mkoa ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
- Kupitia na kutoa taarifa juu ya udhibiti sahihi wa mapokezi, utunzaji na matumizi ya rasilimali fedha za Mkoa
- Kupitia na kutoa taarifa juu ya kiutendaji na kuandaa taarifa za fedha na nyinginezo.
- Kupitia na kutoa taarifa juu ya mifumo iliyopo inayotumika kutunza rasilimali na kujiridhisha uwepo wa rasilimali hizo husika
- Kupitia na kutoa taarifa juu ya majibu ya menejimenti kwenye taarifa za ukaguzi wa ndani na kuisaidia menejimenti kwenye utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa kwenye taarifa mbalimbali na ufutiliaji kwenye utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
- Kupitia na kutoa taarifa juu ya uwezo/ufanisi wa udhibiti uliopo kwenye mifumo iliyounganishwa na kompyuta kwenye Sekretarieti ya Mkoa.
- Kuandaa na kutekeleza Mipango Mkakati wa Ukaguzi wa Ndani.