Idara ya Uchumi na Uzalishaji ina lengo la kutoa uwezeshaji wa kitaalamu kuhusu sekta za uchumi na uzalishaji kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa. Idara hii inaongozwa na Afisa Mkuu Uchumi na Uzalishaji ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa
Majukumu ya Idara ya Uchumi na Uzalishaji:
- Kuratibu utekelezaji wa sera za Kilimo, Mifugo, Ushirika, Misitu, Uhifadhi, Uvuvi, Viwanda, Biashara na Masoko katika Mkoa
- Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa katika kutoa huduma kwenye nyanja za Kilimo, Mifugo, Ushirika, Misitu, Uhifadhi, Uvuvi, Viwanda, Biashara na Masoko
- Kuzisaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya teknolojia zinazofaa na za gharama nafuu katika sekta za uchumi na uzalishaji
- Kusajili vyama/vikundi vya ushirika katika Mkoa
- Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika juu ya uanzishaji/uimarishaji na ukaguzi wa vyama vya Ushirika na Akiba na Mikopo
- Kusaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya kuwasimamia wajasiriamali
- Kuzisaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutambua maeneo nyeti ya uwekezaji
- Kuzisaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza na kukuza sekta ya uvuvi na kuzalisha kisasa
- Kusimamia, kuratibu na kuwezesha masuala yanayohusiana na misitu katika Mkoa
- Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kusimamia utalii katika Mkoa
- Kutoa ujuzi wa kitaalamu kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye masuala yanayohusiana na maeneo/miradi ya umwagiliaji
- Kuratibu utekelezaji wa uboreshaji wa taratibu za biashara katika Mkoa.