OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Matangazo>>Tangazo la Kujiunga na JKT
Matangazo

Tangazo la Kujiunga na JKT

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi anawatangazia na kuwataka vijana wote wakaazi wa Mkoa wa Mjini Magharibi kutuma maombi yao ya kujiunga na jeshi la kujenga taifa (JKT) kwa utaratibu wa kujitolea kwa hiari kwa mkataba wa miaka miwili (02) ya kulitumikia Taifa.

Muombaji anatakiwa awe na sifa zifuatazo

 1. Awe raia wa tanzania
 2. Umri.
 3. Kwa vijana wenye elimu ya darasa la saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18.
 4. Vijana wenye elimu kidato cha nne umri usiwe zaidi ya miaka 20.
 5. Vijana wenye elimu ya kidato cha sita umri usiwe zaidi ya miaka 22.
 6. Vijana wenye elimu ya stashahada umri usiwe zaidi ya miaka 25.
 7. Vijana wenye elimu ya shahada umri usiwe zaidi ya miaka 26
 8. Vijana wenye elimu ya shahada ya uzamili umri usiwe zaidi ya miaka 30
 9. Vijana wenye elimu ya shahada ya uzamivu umri usiwe zaidi ya miaka 35.
 10. Awe na afya njema, akili timamu na asiwe na alama ya michoro mwilini (tattoo)
 11. Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia mahakamani na hajawahi kufungwa.
 12. Kwa vijana waliomaliza elimu ya sekondari kidato cha nne na sita wawe waliomaliza kuanzia mwaka 2019, 2020, 2021 na 2022 wenye ufaulu ufuatao;-
 13. Vijana kidato cha nne wawe wamefaulu na wawe na alama (points) zisizopunguwa 32.
 14. Vijana kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la nne.
 15. Awe na elimu ya msingi aliyehitimu darasa la saba.
 16. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa na (original birth certificate)
 17. Awe na awe na cheti halisi cha kumalizia shule (school leaving certificate)
 18. Awe na awe na cheti halisi cha matokeo (original academic certificate/ transcript).
 19. Asiwe ametumikia jeshi la polisi, magereza, chuo cha mafunzo au kmkm wala kuajiriwa idara nyengine serikalini.
 20. Asiwe na amepitia jkt operesheni za nyuma .
 21. asiwe amejihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na yanayofanana na hayo.
 22. Kwa wale wenye vipaji vya michezo mbali mbali vya sanaa sifa za elimu ni sawa na zilizotajwa hapo juu.

Wale wote watakaomba wanatakiwa kuwasilisha maombi yao katika Ofisi za Wilaya wanazoishi.

Mwisho wa kupokea maombi hayo ni tarehe 05/09/2022 saa 09:30 alasiri.

Tanibihi;-

Ikumbukwe kuwa vijana wote watakaojiunga na JKT kwa kipindi cha miaka miwili (02) ni kwa lengo la kujitolea na si kwa nia ya kuajiriwa na JKT au kutafutiwa ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama, Serikali,  Taasisi za Kimataifa, Asasi au Mashirika binafsi.