OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Miradi ya Maji yaondoa tatizo la ukosefu wa Maji Safi na Salama Mkoa Mjini Magharibi
HabariHabari Mpya

Miradi ya Maji yaondoa tatizo la ukosefu wa Maji Safi na Salama Mkoa Mjini Magharibi

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa ameishukuru bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA kwa juhudi zake za kusimamia na kutekeleza vyema miradi ya maji safi na salama katika mkoa wa Mjini Magharibi.

Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo alipokutana na ujumbe wa bodi hiyo waliofika ofisini kwake kwa ajili ya tathmini ya utekelezaji majukumu ya miradi ya maji kwa kipindi cha miaka 3 tangu kuundwa kwa bodi hiyo.

Amesema kuwa juhudi kubwa zilizofanywa na bodi hiyo zimeleta mafanikio yaliyotarajiwa ambapo mkoa huo umekuwa ni mnufaika mkubwa wa miradi ya maji ambayo imeondoa tatizo la ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi wake.

Aidha Mhe Idrissa amewata wasimamizi na watendaji mbalimbali kuwa makini na watu wasio na nia njema na Serikali ambao wanaharibu miundombinu ya maji hali inayorudisha nyuma hatua za maendeleo zilizopo. 

Hata hivyo Idrissa ameihakikishia bodi hiyo kuwa mkoa wake kupitia kamati ya Ulinzi na Usalama utahakikisha kuwa unasimamia kwa karibu   usalama wa wananchi pamoja na kulinda miundombinu hiyo kwa kuwadhibiti wale wote wenye nia ya kuharibu miundo mbinu hiyo.

Mapema Mwenyekiti wa Bodi hiyo Balozi Mstaafu Meja Jeneral Issa Suleiman ameeleza mafanikio makubwa yaliopatikana ikiwemo ukamilishaji wa miradi yote ya maji sambamba na ujenzi wa jengo la afisi ya Mamlaka ya Maji Zawa.

Akielezea taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo Mkurugenzi Biashara na huduma kwa wateja Asma Ahmed Mahamoud amesema jumla ya mita elfu kumi na tatu, mia mbili na arobaini na tano (13,245) za maji tayari zimeshafungwa kwa wananchi kwa njia ya mkopo ili kuhakikisha   wananchi wanapata huduma hiyo

Asma ameongeza kuwa jumla ya mita ishirini na saba elfu zilizopo ambazo zinahitaji jumla ya shilingi bilioni moja zitafunwa kwa wananchi katika maeneo yaliobalki mara tu baada ya kuipata fedha hiyo kutoka serikalini.