Idara hii lengo lake ni kutoa huduma za kitaalamu katika nyanja za Mipango, Bajeti na vilevile kuratibu shughuli za Kiserikali Mkoani. Idara hii inaongozwa na Afisa Mkuu Mipango na Uratibu anayewajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Idara ya Mipango na Uratibu:
- Kuratibu suala zima la maendeleo ya kiuchumi kwenye Mkoa ikijumuisha Sekta Binafsi, Mashirika ya Serikali, Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na Asasi za kijamii.
- Kuratibu Shughuli za kitaifa katika ngazi ya Mkoa
- Kufuatilia utekelezaji wa ahadi za viongozi wakuu wa Nchi wakati wa ziara na ilani ya uchaguzi
- Kushauri na kuratibu utekelezaji wa sera za sekta mbalimbali katika Mkoa
- Kuratibu maandalizi, usimamizi na tathimini ya mipango (Mpango Mkakati, Mpango Kazi na Bajeti) kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa
- Kuratibu mikutano ya Kamati ya Ushauri ya Mkoa
- Kuchambua, kuunganisha na Kusimamia maandalizi na utekelezaji wa Mpango wa Sekretarieti ya Mkoa na Bajeti
- Kuratibu miradi inayofadhiliwa na wafadhili/wadau wa maendeleo na kushauri shughuli za utekelezaji wa Miradi.
- Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa kuhusu shughuli na majukumu ya mashirika, taasisi za kijamii na sekta binafsi
- Kushauri na kuratibu shughuli za utafiti katika Mkoa
- Kuratibu mazoezi ya sensa ya watu na makazi
- Kuzisaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuandaa maandiko ya miradi
- Kuratibu utekelezaji na kusimamia ushiriki wa sekta binafsi katika masuala mbalimbali ya maendeleo
- Kusimamia na kutathimini utendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa.