OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Dr. Mwinyi awataka mabalozi kuitangaza Zanzibar na fursa za Kiuchumi
Habari

Dr. Mwinyi awataka mabalozi kuitangaza Zanzibar na fursa za Kiuchumi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka Waheshimiwa Mabalozi walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali Duniani kuitangaza Zanzibar na kutafuta fursa za kiuchumi.

Fursa hizo zilizopo kwenye uchumi wa buluu ikiwemo sekta ya utalii kwa maeneo ya uwekezaji kwenye utalii wa fukwe, urithi, fursa za uwekezaji kwenye utalii wa mikutano na michezo, fursa za uwekezaji katika sekta ya uvuvi kwenye ufugaji wa viumbe vya bahari pamoja na ukulima wa mwani, sekta ya bandari eneo la bandari ya makontena , nafaka na chelezo, fursa za uwekezaji wa mafuta na gesi , upatikanaji wa meli za usafirishaji wa mizigo na abiria, ufadhili wa masomo, fursa za masoko ya bidhaa za ndani , upatikanaji wa fedha kwa njia ya mikopo au misaada ili kuweza kufanya miradi ya maendeleo, kuimarisha ushirikiano wa ujirani mwema na fursa za kibiashara pamoja na ulinzi na usalama.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 04 Oktoba 2023 akizungumza na Waheshimiwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali akiwemo Balozi Khamis Omar-Beijing, China, Balozi Hassan Mwamweta-Berlin, Ujerumani, Balozi Dkt. Bernard Kibesse-Nairobi, Kenya, Balozi Mej.Jen. Ramson Mwaisaka-Cairo, Misri, Balozi Gelasius Byakanwa-Bujumbura, Burundi, Balozi Habibu Mohamed-Doha, Qatar, Balozi Imani Njikai-Algeirs, Algeria, Balozi Dkt.Mohamed Juma Abdallah-Riyadh, Saudia Arabia waliofika Ikulu kujitambulisha na kumuaga.