OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Bilioni 50 kutumika kufanya ukarabati Beit el Ajaib
HabariHabari Mpya

Bilioni 50 kutumika kufanya ukarabati Beit el Ajaib

Kiasi cha shilingi bilioni 50 sawa na dola za kimarekani milioni 21 zitatumika katika ukarabati wa  Jengo la Bait el ajaib lililopo forodhani.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe Ali Said Bakari huko ofisini kwake Forodhani alipokuwa akizungumzia kuhusu ukarabati wa jengo hilo.

Amesema  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale tayari imeshatiliana saini mkataba wa ujenzi wa mradi huo na Serikali ya  Oman  mwezi febuari 2023.

Ameeleza kuwa ukarabati wa jengo hilo  utafanywa na kampuni ya Nadhra ya Dar es salaam ambayo itakabidhiwa kazi hiyo hivi karibuni  na inatarajiwa kukamilika  ndani ya kipindi cha miaka mitatu.

Takriban miaka miwili na nusu tangu jengo hilo la kihistoria  lilipoanguka mwezi Disemba mwaka 2020 wakati ukarabati wake ulikuwa umeanza kufanyika.