Idara hii lengo lake ni kuwezesha utoaji wa huduma bora za Ustawi wa Jamii katika Mkoa. Idara hii inaongozwa na Afisa Mkuu Huduma za Jamii ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Idara ya Huduma za Jamii:
- Kuratibu masuala ya Ustawi wa Jamii katika Mkoa
- Kusikiliza changamoto za wananchi wanaofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
- Kusimamia Mikakati na sera za elimu
- Kusimamia masuala Mtambuka ikiwemo Ulemavu n.k
- Kutoa huduma za msaada unaohitajika wakati wa milipuko ya magonjwa katika Mkoa