OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Tawala kucheza fainali ya Mapinduzi cup
HabariHabari Mpya

Tawala kucheza fainali ya Mapinduzi cup

Timu ya Wizara ya Nchi (AR) Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ imefuzu kucheza fainali za mashindano ya kombe la Mapinduzi kwa timu za Wizara na taasisi za Serikali.

Tawala iliitandika Wizara ya Nchi (AR) Fedha na mipango mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa Mao se Tung

Ilichukua dakika tano tu ya kipindi cha kwanza kwa Tawala kutingisha nyavu za Fedha kwa bao safi lililofungwa na Muumin Ali. Dakika ya 21 fedha ilisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Juma Suleiman.

Dakika ya 55 kipindi cha pili Tawala ilifanikiwa kupata bao la pili lililoipeleka fainali lilofungwa na kiungo wake Shaaban Khamis baada ya kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa fedha.

Akizungumza na wachezaji wa Tawala baada ya mchezo huo Mrajis wa Jumuia zisizo za Serikali Zanzibar kwa niaba ya Wizara Ahmed Khalid Abdalla amewapongeza viongozi na wachezaji kwa kufanikiwa kuingia fainali ya mashindano hayo.

Amesema Wizara itaendelea kutatoa kila aina mashirikiano ili kuona mikakati ya timu hiyo kuchukua ubingwa inatimia.