OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI

Home>>Habari>>Mkuu wa Mkoa asifu mashirikiano ya wafanyakazi
HabariHabari Mpya

Mkuu wa Mkoa asifu mashirikiano ya wafanyakazi

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa amewaasa wafanyakazi wa Afisi yake kuendeleza mashirikiano katika utendaji wao wa kazi

Amesema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi katika kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mhe. Idrissa ameeleza kuridhishwa na utendaji wa wafanyakazi wa Ofisi hiyo na kuwahimiza waongeze bidii ili kufikia malengo ya Serikali.

Aidha Mkuu wa Mkoa amewatakia Wafanyakazi hao kheri ya Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa alitoa sadaka ya futari kwa wafanyakazi wa Ofisi yake.